Saturday, September 14, 2013

DIAMOND APINGA TUHUMA YA KUIBA BEAT YA WIMBO WA DYANA


Siku chache zilizopita msanii Dyana ambaye ametamba sana na wimbo wa “nivute kwako” alisema Diamond ametumia beat ya wimbo wake bila taarifa yoyote.

Beat ya my number one wa Diamond ndio beat Dyana analalamika kwamba Diamond katumia beat yake bila taarifa yoyote. Na huu ndio wimbo ambao Dyana anadai kwamba Diamond kaiba beat

Diamond Platnumz alimwambia Dyana kwamba asimpe lawama bali anachotakiwa kufanya ni kuongea na Sheddy Clever ambaye ni mtayarishaji wa ngoma yangu My Number 1.

SAMSUNG : SMARTPHONE HAITOSHI, SASA SMARTWATCH


Siku chache zilizopita mabingwa wa smart phone Samsung walizindua saa ya kwanza ambayo wameipa jina la Galaxy Gear smartwatch.
Galaxy Gear smartwatch ina 1.63-inch OLED screen na mikanda ya mpira. Kwenye hiyo saa unaweza kupiga simu bila kuasahau apps ambazo zipo ndani ya simu.

Kitu kikali kabisa katika saa hiyo ni uwezo wa kujua kama kuna email au message mpya katika simu yako.

NIKK MBISHI – ASIKITISHWA NA WEBSITE ZINAZOTOA HABARI ZA UONGO.


Msanii wa Hip hop Nikk Mbishi amesikitishwa na baadhi ya mitandao ya hapa Bongo kuzusha Habari pasipo uthibitisho.
Nikk Mbishi alifunguka baada ya kukutana na mwandishi wa Baabkubwa, baada ya kuzushiwa amejitangaza ana ‘UKIMWI’.

“Ukweli baadhi ya website za hapa Bongo zipo kimagumashi tu maana zinazusha jambo ambalo halipo na ata kama lipo Ukimwi hauwi sana kuliko maralia inavyouwa may be ningeambiwa na Maralia ingekuwa sawa coz ukichelewa kutibiwa unakufa faster, so wenye Website wawe makini na kile wanachofanya.” 

YANGA YAPEWA SIKU 14 KUWALIPA NSAJIGWA NA MWASIKA.


Yanga imepewa siku 14 kuanzia leo (Septemba 13 mwaka huu) kuwalipa waliokuwa wachezaji wake msimu uliopita, nahodha Shadrack Nsajigwa na Stephen Mwasika wanaoidai klabu hiyo jumla ya sh. milioni 15.5.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Septemba 12 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine ilisikiliza madai ya wachezaji hao.

Fedha hizo ni ada ya usajili ambayo klabu hiyo ilikubaliana na wachezaji hao wakati ikiwasainisha mikataba. Yanga imeshawalipa sehemu ya fedha walizokubaliana na kiasi hicho ndicho bado hakijalipwa. Nsajigwa anadai sh. milioni 9 wakati Mwasika ni sh. milioni 6.5.